Sunday, February 7, 2016

Wanawake/Wasichana Na Karate

Latifa Alberto ndio msichana pekee alikuwa katika mitihani ya madaraja ya mkanda mweusi. Akifanya mtihani wake wa Shodan (Daraja La Kwanza L a Mkanda Mweusi) na kufanya vizuri kabisa kati ya wenzake wa daraja hilo, anajiunga na wasichana/wanawake wachache sana Tanzania walioweza kufika daraja hilo kwa uwezo wao wa kweli.
Kwa kufanya vizuri hivyo na kwakuwa msichana/mwanamke pekee katika mitihani hiyo Shihan Dr. P. Chikoko alimzawadia mkanda mweusi mpya kabisa kama zawadi na motisha ya yeye kuendelea kufanya vizuri na kutokukata tamaa kwa vikwazo vichache anavyokutana navyo katika sanaa au nje ya sanaa vikihusisha sanaa
Pia ikumbukwe kuwa Latifa Alberto Ndie mwalimu anaefundisha karate shule ya Sekondari ya wasichana Feza (Feza Girls Kawe)

Akivua Mkanda wake wa zamani Wa Kahawia (Brown Belt) kwa ajili ya mkanda wake mpya

akivalishwa mkanda wake mpya wa daraja lake jipya


akitoa shukran kwa Shihan Chikoko

No comments: